Design & Creativity
Hiki ndicho kiini cha website nzuri zinazovutia. Tutajifunza japo kwa ufupi jinsi gani unaweza kuboresha ubunifu wako na baadhi ya software na principles za kutumia.
Internet & Website zinafanyaje kazi
Hapa tutazama kwa mapana jinsi internet na website zinavyofanya kazi. Hii ni muhimu ili kuelewa namna bora za kutatua matatizo pamoja na kutumia vyema resources za mtandao.
Website Bora zikoje
Hapa tutajifunza kwa mifano hai website bora zikoje. Nini sifa ya website bora na jinsi gani inavyoweza kutengenezwa.
Jinsi ya kutengeneza website kwa kutumia Wordpress
Tutafahamu kila kitu kuhusu Worpress, ni nini, inatumikaje, kwanini nasema ni rahisi? Tutajifunza mbinu bora za kutengeneza website za viwango vya hali ya juu na kuwafurahisha wateja wako ndani ya mida mfupi.
Jinsi ya kuongeza ulinzi, kupatikana katika search engine na kutunza website
Tutajifunza mbinu bora za kulinda website kutoka kwa mashambulizi mbalimbali mtandaoni. Pia tutaona mbinu za kupatikana vizuri katika Search Engines mbalimbali na namna gani ufanye website iwe na manufaa kwako na wateja wako.
Jinsi ya kupata kipato kwa kutumia ujuzi huu
Tutajifunza jinsi ya kunufaika na taaluma hii. Jinsi ya kujiweka katika soko na kupata wateja pamoja na kumonetize website yako ili ikuingizie kipato.